Home Uncategorized MBEYA CITY HAWANA BAHATI NA BOCCO UWANJA WA SOKOINE

MBEYA CITY HAWANA BAHATI NA BOCCO UWANJA WA SOKOINE

 


JOHN Bocco, nahodha wa Simba ndani ya misimu miwili mfululizo ameiadhibu Mbeya City na kuipa timu  yake pointi tatu muhimu. 


Msimu wa 2019/20 wakati Simba ikishinda mabao 2-0 Uwanja wa Sokoine na kusepa na pointi tatu, Bocco alitupia mabao yote mawili.


Msimu huu pia wa 2020/21 wakati Simba ikishinda bao 1-0, Bocco alitupia bao la ushindi na kujenga ushkaji na Uwanja wa Sokoine kila wakutanapo na Mbeya City. 


Ndani ya misimu miwili, Bocco amewaadhibu Mbeya City nyumbani kwa juma ya mabao matatu ambayo yamefanya Simba ikusanye jumla ya pointi sita.


Ushindi wa jana, Desemba 13 unaifanya Simba kufikisha pointi 29 na kuishusha Azam FC nafasi ya pili kwa kuwa ina pointi 27 na imecheza mechi 14 leo ina kazi mbele ya Namungo FC.

SOMA NA HII  YANGA KUMENYANA KESHO NA KAGERA SUGAR USIKU