Home Ligi Kuu BIASHARA UNITED YATAKA KUFANYA BIASHARA NA SIMBA

BIASHARA UNITED YATAKA KUFANYA BIASHARA NA SIMBA


 FRANCIS Baraza,Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa wamejipanga kupata pointi tatu mbele ya wapinzani wao Simba kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Februari 18, Uwanja wa Karume.

Ikiwa lengo la Baraza litafanikiwa itakuwa imefanya biashara ya kusepa na pointi tatu mbele ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Biashara United inakumbuka kwamba mzunguko wa kwanza ilipoteza pointi tatu mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 4-0, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo wao wa mwisho  ndani ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC  hivyo itaingia ndani ya uwanja kwa kujiamini.

Kocha huyo ambaye mkononi ana tuzo ya kocha bora wa mwezi januari amesema kuwa wanahitaji pointi tatu kutoka kwa Simba.

“Ninawaamini wachezaji wangu na tayari maandalizi yameanza kwa ajili ya mchezo wetu muhimu ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Ninawatambua wapinzani wetu Simba namna ambavyo wanacheza pamoja na ubora wao, hatutawabeza tutawaheshimu, ina wachezaji wazuri ila wajue kwamba hata sisi tuna wachezaji wazuri,” .

Biashara United ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 32 na Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 39. 

SOMA NA HII  SIMBA YAINGIA MAKUBALIANO NA VUNJA BEI LEO