Home Yanga SC METACHA ATAJWA KUJIWEKA KANDO NDANI YA KIKOSI CHA YANGA

METACHA ATAJWA KUJIWEKA KANDO NDANI YA KIKOSI CHA YANGA

 


IMEELEZWA kuwa kipa namba moja wa Klabu ya Yanga, Metacha Mnata amejiweka kando ndani ya klabu hiyo kutokana na matokeo mabovu ambayo wamekuwa yakipatikana ndani ya timu hiyo.

Mnata jana, Machi 7 alikuwa langoni wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Sare hiyo imewafanya Yanga wabaki nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 50 kibindoni huku Polisi Tanzania ikiwa nafasi ya 8 na pointi zake 29.

Bao hilo alilofungwa dakika ya 89 kwa kichwa cha mchezaji wa zamani wa Yanga, Pius Buswita jambo ambalo liliwafanya malengo ya kusepa  jumla na pointi tatu kuyeyuka jumla.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh ameweka wazi kwamba bado hajapata taarifa hizo kwa kuwa wachezaji walioitwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars walielekea kambini.


 

SOMA NA HII  KASEKE, FEI TOTO WAWEKA REKODI YAO KWA MKAPA