Home Uncategorized HIKI HAPA KILIMPOTEZA MUUAJI WA YANGA JUMLA KWENYE LIGI

HIKI HAPA KILIMPOTEZA MUUAJI WA YANGA JUMLA KWENYE LIGI

SALIM Aiyee, nyota wa KMC msimu uliopita wa 2018/19 wakati akikipiga ndani ya Mwadui FC alimaliza Ligi Kuu Bara akiwa namba moja kwa wazawa kucheka na nyavu akiwa na mabao 19.

Msimu huu 2019/20 Aiyee amepachika bao moja pekee alilowatungua Yanga kwenye mechi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, Machi 12.

Kwa sasa kinara wa mabao ndani ya ligi ni Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 19 huku wazawa ni Reliants Lusajo wa Namungo Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar na Paul Nonga wa Lipuli wametupia mabao 11.

Aiyee amesema kuwa sababu ya kushindwa kufanya makubwa msimu huu ni kusumbuliwa na majeraha ambayo yalimkalisha nje ya Uwanja muda mrefu.


KMC ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 33 imecheza mechi 29 za Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  JEMBE LA KAZI LIMERUDI MAZIMA YANGA