Home news PAMOJA NA KUWA HATAKUWA KWENYE BENCHI…NABI AFUNGUKA NAMNA WATAKAVYOMSULUBISHA MNYAMA…

PAMOJA NA KUWA HATAKUWA KWENYE BENCHI…NABI AFUNGUKA NAMNA WATAKAVYOMSULUBISHA MNYAMA…


YANGA imeingia kambini jana mchana tayari kwa maandalizi dhidi ya Simba lakini kocha wao Nasreddine Nabi ametamka kwamba watashuka na mambo mapya ndani ya mchezo huo.

Nabi ambaye hatakaa benchi katika mchezo huo wa Jumamosi kutokana na adhabu, alisema baada ya kuwa na wachezaji wake wote walio timamu kucheza mchezo huo sapraizi ya kwanza itakuwa upangwaji wa timu.

Kocha huyo alisema ana uhakika wa kumkosa mchezaji mmoja pekee katika timu yake – mshambuliaji Yacouba Sogne, lakini wengine wote wako tayari kwa mchezo huo.

“Tuna timu kamili nafikiri hii itakuwa sapraizi ya kwanza sijajua tumtumie mchezaji gani kuelekea mechi hii. Kila mtu yuko tayari na wachezaji wanataka kucheza hii mechi,” alisema Nabi ambaye juzi alipewa gari mpya aina ya Toyota Vanguard na uongozi wa GSM.

“Tutamkosa Yacouba (Songne) pekee, lakini tuna nafasi kubwa ya kuchagua watu bora ambao tutawaona wako tayari kutupa ushindi. Hii ni mechi ambayo tunatakiwa kushinda kwa namna yoyote.”

Kocha huyo aliongeza kuwa kama kuna kitu kigumu kitawaumiza wao kama makocha ni kuchagua wachezaji ambao watacheza eneo la kiungo ambapo hii inaweza kuwasaparaizi hata wachezaji wenyewe mbali na mashabiki.

Alisema kupona kwa Feisal Salum na Khalid Aucho kunawafanya sasa viungo hao kuungana na wenzao waliokuwepo Salum Aboubakar ‘Sure boy’ Zawadi Mauya na Yannick Bangala ambaye ni kipenzi cha mashabiki.

Alisema sambamba na hilo pia kuna kazi ya kuchagua mawinga wa pembeni ambao nao kila mmoja yuko tayari kucheza mechi hiyo ambayo itawapa nafasi zaidi ya kwenda kuwa mabingwa endapo watashinda au kupata sare.

“Kuna kazi kubwa kuchagua viungo wa kucheza hiyo mechi nafikiri hili ndio gumu zaidi, tutakuwa tofauti zaidi nilisema kabla kwamba ubora wetu uko katika eneo la kiungo, na kurejea kwa Aucho na Feisal kunaleta nguvu zaidi kwenye timu yetu.

“Nilifurahi kuona mchezo uliopita (dhidi ya Namungo) Feisal na Aucho walimaliza vizuri bila kuonekana shida ya afya yao hii ni nafasi nyingine ya kupata timu iliyokamili,” aliongeza Nabi ambaye timu yake inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 54 ikifuatiwa na Simba yenye 41.

SOMA NA HII  BAADA YA KUNUSURIKA KUSHUKA DARAJA...MTIBWA SUGAR WATIMUA MASTAA ZAIDI YA 20...TIMU YA VIJANA WALA SHAVU..