Home news KUELEKEA YANGA vs SIMBA…MWAMUZI WA KATI HUYU HAPA…JINA LAKE LAPATIKANA USIKU WA...

KUELEKEA YANGA vs SIMBA…MWAMUZI WA KATI HUYU HAPA…JINA LAKE LAPATIKANA USIKU WA MANANE…


JOTO la mpambano wa Ligi Kuu Bara baina ya Yanga na Simba utakaopigwa Jumamosi saa 11 jioni wiki hii katika Uwanja wa Mkapa linazidi kupanda.

Hii sio tu kwa mabosi wa timu hizo, ila hata mashabiki wao.

Lakini kuna tukio kubwa lililojiri jijini Dar es Salaam jana usiku. Vigogo wa waamuzi na Bodi ya Ligi walikutana kuchekecha majina matano kupata moja la refa atakayesimama katikati Jumamosi.

Ni mchezo mgumu na wenye ushindani wa aina yake ambao tangu jana Simba na Yanga zimekuwa na hamu ya kujua nani atakuwa mwamuzi wa kati na hata wale wa pembeni.

Licha ya kwamba viongozi hao wa waamuzi wanafanya siri kubwa lakini habari za uhakika  ni kwamba mpaka wanaanza kikao jana mezani kulikuwa na majina matano.

Lakini kuna wawili wanaopewa nafasi kubwa, Eli Sasii na Abdalah Mwinyimkuu.

Sasii aliamuru kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Desemba 11 wakati timu hizo zikitoka suluhu Simba akiwa mwenyeji.

Mwinyimkuu yeye anatoka Singida naye yupo kwenye orodha akipewa nafasi kubwa. Wengine ni Hance Mabena, Emmanuel Mwandembwa na Abel William ambae moja ya mchezo alioamua ni ule ya Namungo na Yanga kule Ilulu, Lindi.

Hata hivyo chanzo cha kuaminika kilieleza licha ya waamuzi hao kupewa asilimia kubwa ya mmoja wao kupewa nafasi ya kuchezesha kikao cha kamati ya waamuzi ndicho kitaamua lakini ni nadra kuwa na sapraizi nje ya hapo. “Kikao cha Kamati ya Waamuzi kitakutana na Jumatano (leo) watangaze,”kilidokeza chanzo chetu cha kuaminika ndani ya waamuzi hao ingawa viongozi jana walikuwa wanarushiana mzigo juu ya nani atapewa hukumu hiyo.

“Safari hii kumekuwa na mvutano mkubwa wa nani atakayeamua mchezo huu kama unavyojua timu zetu na soka letu lilivyo ndani yake kuna mambo mengi.”

Hata hivyo katika michezo mitano iliyopita ya Ligi Kuu Bara zilipokutana timu hizo hakuna mwamuzi aliyechezesha dabi zote mbili za msimu au kujirudia, japo lolote linaweza kujitokeza msimu huu kutokana na changamoto za waamuzi na ushindani uliopo.

SOMA NA HII  TAKWIMU ZINAONGEA....YANGA WAKIKAZA WANATOBOA ROBO FAINAL SHIRIKISHO CAF...