Home Simba SC KOCHA SIMBA: NAMJUA VIZURI IBENGE, NINAJIAMINI

KOCHA SIMBA: NAMJUA VIZURI IBENGE, NINAJIAMINI

 



MFARANSA Didier Gomes ambaye ni kocha mkuu wa Simba ametamba kwamba anajiamini mbele ya mpinzani wake kocha wa AS Vita, Florent Ibenge kwa kuwa anamjua vizuri kwa namna ambavyo anafundisha.

Wawili hao wataziongoza timu zao katika kupambana kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ya Kundi A ambayo itapigwa leo Ijumaa nchini DR Congo kwenye Uwanja wa Martyrs de la Pentecote.

Mara ya mwisho walipokutana msimu wa 2018/19 jijini Dar Simba walishinda kwa mabao 2-1 na kutinga robo fainali ambayo walifungwa na TP Mazembe kwa mabao 4-1.

Gomes ameliambia gazeti la Championi Ijumaa, kuwa anamjua vyema Ibenge kuwa ni kocha mzuri na anayependa ‘fair’ lakini hata hivyo yeye anajiamini kutokana na aina ya kikosi ambacho anacho.

 “Namjua vizuri kocha wao Ibenge, ni mtu mwema, ambaye amekuwa na fair ukikutana nae pia yuko safi lakini hata hivyo kwangu mimi ninajiamini zaidi kwenye mechi hii.“Tumefanya maandalizi mazuri ya mechi hii na nimewaambia baadhi ya makosa kwenye mazoezi yetu lakini nimewasisitiza zaidi kwenye suala la kufunga hata kwenye nafasi moja tu kwani hatuwezi kupata nafasi nyingi,” aliweka nukta Gomes

Stori na Said Ally, Dar es Salaam

SOMA NA HII  SIMBA: KAMBI YA MOROCCO IPO VIZURI,JEZI MPYA KUTAMBULISHA