Home Yanga SC CARLINHOS ATAMBA KUENDELEA KUUWASHA MOTO YANGA

CARLINHOS ATAMBA KUENDELEA KUUWASHA MOTO YANGA


BAADA ya kuipa Yanga pointi tatu muhimu katika mchezo wa jana dhidi ya Mtibwa Sugar, kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Angola, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ amesema kuwa amejipanga vizuri kuisaidia timu yake baada ya kurejea kutoka kwenye majeruhi.

Carlinhos alifunga bao hilo dakika ya 73 ya mchezo akimalizia pasi ya Mkongomani Tuisila Kisinda, dakika moja tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya Ditram Nchimbi.

Bao hilo linamfanya Carlinhos aliyekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu mpaka sasa awe amehusika kwenye mabao matano ya Yanga msimu huu akifunga mabao matatu na kuasisti mara mbili.

Akizungumzia uwezo wake kwenye mchezo huo Carlinhos amesema: “Nimefurahi kuona narejea kwa kasi baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuwa na majeraha.

“Ushindi huu umezidi kunipa nguvu ya kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo na naamini nitafunga na kujitahidi kutengeneza mabao mengi zaidi kwa ajili ya mafanikio ya kikosi changu,”

SOMA NA HII  KISA SIMBA...VIGOGO WAVAMIA KAMBI YA YANGA KIGAMBONI..MAKAMBO ATOBOA SIRI A-Z.....DK MSOLA 'ALIA'..