Home Habari za michezo MAYELE AFICHUA ALIVYOPIGA SIMU KUOMBA KUJIUNGA YANGA…AFUNGUKA STAILI YAKE KUTUMIKA KANISANI…

MAYELE AFICHUA ALIVYOPIGA SIMU KUOMBA KUJIUNGA YANGA…AFUNGUKA STAILI YAKE KUTUMIKA KANISANI…


Top scorer wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Fiston Kalala Mayele amefunguka namna alivyosajiliwa Yanga na kufanikiwa kuipa manufaa makubwa timu hiyo mpaka sasa.

Akizungimzia hilo, Mayele ambaye ni raia wa Congo DR amesema wachezaji wenzake waliokuwa Yanga, Tonombe Mukoko na Tuisila Kisinda ndio walimshawishi yeye kujiunga na Wananchi wa Jangwani.

“Kisinda na Mukoko ndio walinishawishi nije Yanga, sana Kisinda aliniambia kuna shida ya Straiker Yanga naomba uje akanipa namba ya Eng Hersi mkataba wangu ulipoisha AS Vita nikamtafuta Hersi tukaongea tukasaini Mkataba wa Miaka miwili.

“Niliwaambia Viongozi wa Yanga wanitafutie nyumba ambayo itakuwa na sehemu ya Gym, naishi Masaki kila asubuhi nafanya Mazoezi yangu halafu jioni naenda Avic Town kwa ajili ya mazoezi ya timu.

“Mapokezi yamekuwa makubwa watu wananipenda style yangu imekuwa maarufu hadi makanisani, Watanzania wanapenda sana mpira upendo wanaonioshesha Yanga unanifanya niendelee kupambana kwa ajili ya Timu hii,” Fiston Mayele.

SOMA NA HII  MASTAA HAWA WA YANGA WANAFAA PALE SIMBA KABISA