Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WASAUZI…SIMBA WAJIAPIZA KUFANYA MAAJABU…AHMED ALLY ATIA ‘CHUMVI’…

KUELEKEA MECHI NA WASAUZI…SIMBA WAJIAPIZA KUFANYA MAAJABU…AHMED ALLY ATIA ‘CHUMVI’…


Meneja wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema ni lazima msimu huu klabu hiyo ifike hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Ahmed Ally amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akizungumzia maandalizi ya klabu hiyo kuelekea mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa robo fainali wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika kusini mchezo utakaochezwa Aprili 17, 2020. Uwanja wa Benjamini mkapa Dar es salaam.

“Hii ni robo fainali ya aina yake, iwe mchana iwe usiku, Mnyama safari hii anaenda semi final, tumedhamiria hilo, tumejipanga kwa hilo ndio maana tunataka mashabiki mje kwa wingi.”- amesema Ahmed Ally

Kuhusu maandalizi ya kikosi amethibitisha kuwa tayari kikosi hicho kimerejea jijini Dar es salaam toka jana kikitokea mjini Moshi ambako kilicheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao ulimalizika kwa suluhu (0-0).

Kwa upande wetu kama Simba maandalizi yameshaanza, kikosi kilirudi jana kutoka Moshi. Nawaomba Wanasimba tusahau yaliyotokea Moshi, tuna kikubwa tunapaswa kukipigania dhidi ya Orlando, tunachofukuzia mbele yetu ni kikubwa kwa nchi, tuna kila sababu ya kufanya kila namna tarehe 17 tufanye maajabu.”- Ahmed Ally

SOMA NA HII  MANULA AFUNGUKA HAYA KUHUSU TUKIO ZIMA LA KUZIMIA UWANJANI