Home news WAANGOLA WA NAMUNGO WAKUTWA NA CORONA, WALALAMIKIA HUJUMA

WAANGOLA WA NAMUNGO WAKUTWA NA CORONA, WALALAMIKIA HUJUMA


UONGOZI wa Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola ambao ni wapinzani wa Namungo katika michezo ya mtoano ya kombe la Shirikisho Afrika, umelalamika kufanyiwa hujuma na Watanzania baada ya wachezaji wao watano wa kikosi cha kwanza kutajwa kuwa na maambukizi ya COVID-19.

Kupitia mitandao yao ya kijamii 1de Agosto walitoa taarifa iliyoeleza kama ifuatavyo: “Dakika ya mwisho wachezaji wetu watano wamedhaniwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona kupitia vipimo vilivyoonyesha wana maambukizi.

“Hili limefanyika ili kudhoofisha timu yetu, Watanzania kwa makusudi na dhahiri kabisa wanadai kuwa wachezaji wafuatao wana maambukizi ya COVID-19: Kipa Neblú, mabeki wa kati Bobó na Boni, kiungo Mário na mshambuliaji Mabululu, pamoja na Mratibu wa timu ya Untonesa Sampaio.

“Habari hii ilifika saa saba mchana kwa saa za Tanzania, na italazimisha benchi letu la ufundi kufanya mabadiliko ya kikosi cha wachezaji 11 waliotarajiwa kuanza,”

Ikumbukwe kuwa wakiwa nchini Angola kwa ajili ya mchezo wa kwanza uliopangwa kufanyika Februari 14, mwaka huu nyota watatu wa Namungo na kiongozi mmoja walitajwa kuwa na maambukizi ya Corona na kusababisha sintofahamu iliyopelekea mchezo huo kufutwa.

Baadae kamati maalum ya Shirikisho la soka Afrika (CAF), ilifikia maamuzi ya kuamuru michezo yote miwili kupigwa hapa Tanzania.

SOMA NA HII  BREAKING....MASTAA SIMBA WAONDOLEWA TAIFA STARS...SABABU HIZI HAPA...