Home kimataifa STEVEN GERRAD MWAMBA WA KAZI

STEVEN GERRAD MWAMBA WA KAZI


MWAMBA mmoja mkorofi ndani ya uwanja kwa vitendo jambo lililofanya awe ni shujaa katika mechi ngumu zile za Liverpool anaitwa Steven George Gerrard raia wa England.

Umri wake kwa sasa ni miaka 41 aliletwa duniani Mei 30,1980 na jambo ambalo analifanya kwa wakati huu ni kuifundisha timu ya Rangers ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Scottish.

Alipachikwa jina la Gerrad Final kwa kuwa alikuwa mmaliziaji wa mipango yote inayopangwa ndani ya Liverpool ndani ya Uwanja wa Anfield na hata walipokuwa wakitoka nje.

Pia alikuwa ananyota ya kuibuka kuwa nyota wa mchezo katika fainali nyingi ikiwa ni pamojq na ile fainali ya FA ya mwaka 2006.

Ana tuzo ya mchezaji bora wa England alitwaa mwaka 2009 mataji mawilibya FA Cup 2001 na 2006 akiwa ndani ya Liverpool. 

Pia ana mataji matatu ya League Cup ilikuwa ni 2001,2003 na 2012, lipo jingine la UEFA ilikuwa 2000/01 na UEFA Super Cup ilikuwa 2001/02, 2005/06 pamoja na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa ni 2004/05 yote haya aliyanyanyua akiwa na Liverpool. 

Ni Legend ambaye alicheza jumla ya mechi 538 na alitupia mabao 125 licha ya kuwa alikuwa ni kiungo na sio mshambuliaji halisia.

Katika timu yake ya taifa ya England jumla ni mechi 114 alicheza na kutupia mabao 21 .

SOMA NA HII  BAYERN MUNICH NOMA, WASEPA NA TAJI LA SUPER CUP MARA SITA