Home kimataifa PSG, REAL MADRID ZAWANIA SAINI YA NYOTA RUDIGER

PSG, REAL MADRID ZAWANIA SAINI YA NYOTA RUDIGER


KLABU ya Chelsea imeanza mazungumzo na nyota wake 
Antonio Rudiger na ishu kubwa ni kuhusu kuongeza mkataba wake.

Chelsea imeweka wazi kuwa inahitaji kuona nyota huyo anabaki ndani ya kikosi hicho.

Lakini pia inatajwa kuwa Paris Saint-Germain, (PSG) na Real Madrid zinamtazama kwa ukaribu nyota huyo ili ziweze kunasa saini yake.

Mabosi hao wa Ulaya wapo tayari kumpa dili nyota huyo ambaye dili lake linatarajiwa kumeguka 2022.


SOMA NA HII  FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA YAWEZA KUPIGWA WEMBLEY