Home kimataifa REAL MADRID WAPIGIA HESABU ZA KUINASA SAINI YA LEWANDOWSKI

REAL MADRID WAPIGIA HESABU ZA KUINASA SAINI YA LEWANDOWSKI


ROBERT Lewandowski anatajwa kuwa kwenye hesabau za Real Madrid msimu ujao ikiwa ataondoka ndani ya kikosi cha Bayern Munich msimu huu kwa mujibu wa ripoti.

Nyota huyo amekuwa na ushikaji mkubwa na nyavu ambapo ametupia jumla ya mabao 43 katika mechi 37 ambazo amecheza mpaka sasa ndani ya Bayern inayoshiriki Bundesliga. 

Lewandowski mwenye miaka 32 dili lake limebaki miaka miwili kukamilika ndani ya kikosi hicho ambapo amekuwa akihusishwa kujiunga na Madrid kitambo hata kabla ya kujiunga na Bayern akitokea Borussia 2013.

Kwa mujibu wa Sky Sport ya Ujerumani imeripoti kwamba Bayern watakuwa tayari kumuuza mshambuliaji huyo kwa dau la euro milioni 52 thamani hiyo imeshuka kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Wakala wa Lewandowski, Pini Zahavi imeripotiwa kwamba yeye anaskilizia ofa nono kwa ajili ya mchezaji wake na hata ikiwa ni Real Madrid atamruhusu akacheze kwa makubaliano.

I

SOMA NA HII  KUHUSU DILI LA KUMSAJILI FEI TOTO...AZAM FC WAANZA KUSHIKANA MASHATI...CEO AMKATAA HADHARANI...