Home kimataifa BAYERN MUNICH NOMA, WASEPA NA TAJI LA SUPER CUP MARA SITA

BAYERN MUNICH NOMA, WASEPA NA TAJI LA SUPER CUP MARA SITA


BAYERN Munich imetwaa taji la tisa la German Super Cup jambo ambalo limewafanya wawe na furaha kutimiza jambo lao kwa kuwa ni mara yao ya sita mfululizo kutwaa taji hilo.

Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Borussia Dartmund, Uwanja wa Signal Iduna Park umewafanya waweze kusepa na taji hilo mazima.

Staa wao Robert Lewandowski alitupia mabao mawili kwenye mchezo huo na bao moja lilifungwa na Thomas Muller huku lile la kufutia machozi kwa Dortmund likifungwa na Marco Reus.

Bayern inakuwa ni timu iliyotwaa taji hilo mara nyingi ambayo ni tisa na imeweza kusepa nalo mara sita mfululizo jambo ambalo linawafanya wazidi kujenga ufalme kwenye soka la Ujerumani.

SOMA NA HII  KISA USHINDI DHIDI YA MAHASIMU ZAO...SHABIKI WA ASANTE KOTOKO APAGAWA NA KUVUA NGUO ZOTE ...