Home Simba SC KAMBI NA USAJILI MPYA SIMBA VYAMCHANGANYA GOMES..AFUNGUKA UGUMU ANAOPATA

KAMBI NA USAJILI MPYA SIMBA VYAMCHANGANYA GOMES..AFUNGUKA UGUMU ANAOPATA


KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema kila mchezaji aliyepo kambini anakiwasha kwelikweli na ushindani ni mkubwa.

Gomes amesema amefurahishwa na utayari waliokuwa nao wachezaji wapya ambao wamejiunga na kikosi hicho msimu huu kwani kila mmoja bila ya kujali ni mgeni amekuwa akifanya mazoezi kwelikweli bila mzaha.

“Nimekuwa na mwanzo mzuri wa maandalizi kwani kuanzia mchezaji mpya na wale wa zamani ndani ya timu wamenionyesha wanastahili kuwepo hapa na kama wakiendelea hivi watakuwa wananipa machaguo mengi katika mechi na wakati mgumu wa kuwatumia kwani wote ni bora,” alisema Gomes ambaye msimu uliopita alibeba vikombe vyote vya ndani.

Katika kambi hiyo wachezaji wa Simba hupiga tizi asubuhi na jioni huku wale wapya saba kila mmoja akiwasha moto kulingana na mazoezi ambayo hupangiwa.

Wachezaji wapya ni Henock Inonga Varane, Abdulsamad Kassim, Israel Patrick Mwenda, Pape Ousmane Sakho, Duncan Nyoni, Peter Banda na Yusuph Mhilu kila mmoja ameonyesha kuwa na kiu ya kupewa nafasi zaidi.

Kwenye mazoezi ya asubuhi ambayo husimamiwa na kocha wa viungo, Adel Zrane hufanya yale ya nguvu na mara zote huingia gym ili kutumia vifaa kama baiskeli, kunyanyua vitu vizito, kuruka vihunzi na mengine mengi.

Awamu ya pili mazoezi yanakuwa ni jioni na hufanyika katika uwanja na husimamiwa zaidi na Didier Gomes pamoja na msaidizi wake, Selemani Matola kwani huwa yanahusu kucheza mpira na mbinu zaidi.

Katika mazoezi hayo ya kucheza na mbinu zaidi, hapo ndipo kunakuwa na ushindani wa aina yake kwani kila mchezaji ambaye hupangiwa jukumu la kufanya hutaka kuonyesha kuwa ni bora zaidi ya mwenzake.

Katika eneo la beki wa kati kuna ushindani wa kutosha kati ya Inonga, Pascal Wawa, Joash Onyango, Kennedy Juma, Erasto Nyoni na Ibrahim Ame kila mmoja anafanya kilicho bora na kutaka kuonyesha ni mzuri zaidi ya mwenzake.

Katika eneo la kiungo kuna utamu wa aina yake wa ushindani kwani wale waliokuwepo msimu uliopita kama Jonas Mkude, Said Ndemla, Larry Bwalya, Mzamiru Yassin na wengineo wanashindana vya kutosha na waliongia katika dirisha hili la usajili kama Abdul Samad.

SOMA NA HII  MASAU BWIRE: TUSIDANGANYANE..WALE WASAUZI SIO WEPESI KIIVYO..SIMBA MSIPOJIPANGA NI KILIO TU...

Kwa mawinga wapya wanne Duncan Nyoni, Papa Ousmane Sakho, Banda na Yusuph Mhilu wanapambana vya kutosha kuonyesha kila mmoja alistahili kusajiliwa na anapaswa kupewa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

Ushindani mwingine upo kwa beki wa kulia Shomary Kapombe ameendelea kuwa katika ubora, lakini amekutana na changamoto kutoka kwa Mwenda ambaye amesajiliwa katika dirisha hili na kwenye mazoezi ya awamu mbili aliyofanya licha ya ugeni wake amefanya vizuri.