Home Simba SC MEDDIE KAGERE: HATA WAKISEMA NINA MIAKA 100, WENGINE HAWAFANYI KAMA MIMI

MEDDIE KAGERE: HATA WAKISEMA NINA MIAKA 100, WENGINE HAWAFANYI KAMA MIMI


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hata watu wakimuita ana miaka 100 yeye hajali kwa kuwa anajivunia kuwa na miaka ambayo wengine hawana.

Nyota huyo aliyesepa na tuzo ya ufungaji bora mara mbili mfululizo, msimu wa 2018/19 alipotupia mabao 23 na msimu wa 2019/20 alipotupia mabao 22 msimu uliopita wa 2020/21 alitupia mabao 13.

Kagere alisema:” Naona kuna watu wanajadili kuhusu umri wangu ila mimi sijali hata ukinipa miaka 100 mimi ninapenda kwa sababu wengine hawana miaka hiyo ambayo mimi nanayo.Wapo wengine vijana ila hawafanyi ninayofanya mimi.

“Unajua kila mtu anaweza kuzungumza kuhusu miaka yangu nadhani ni sawa, kila mmoja anaweza kusema nina miaka mingi sawa. Ninajua kwamba kila mtu anakua kwenda mbele na sio kwenda chini. Ikiwa unaniita mimi mzee hilo sijali kwa kuwa kuna kitu ninazalisha. Ikiwa nipo hapa ninaitwa mzee lazima ujiulize nimewezaje kufanya.

“Unajua mpira ni kupanda na kushuka kuna wakati unaanguka na kuna wakati unapanda. Lakini hakuna namna ni maisha ya mpira.Ninajua nani ambaye ananilipa nani ninamfanyia kazi kwa kuwa wao hawajasema mimi ni mzee basi nitaendelea kufanya kazi,” .

Kwa sasa Kagere yupo nchini Morocco na kikosi cha Simba ambacho kimeweka kambi huko kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22.

SOMA NA HII  KIMEUMANA SIMBA....BWALYA HATIHATI....MORRISON NA BOCCO 'OUT'...