Home Ligi Kuu MAXIME AITAJA MIPANGO YAKE BAADA YA KUPIGWA CHINI KAGERA SUGAR

MAXIME AITAJA MIPANGO YAKE BAADA YA KUPIGWA CHINI KAGERA SUGAR


ALIYEKUWA kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amefunguka kuwa hajapokea ofa ya kufundisha timu yoyote mpaka sasa, na hayuko tayari kwa majukumu hayo kwani amejipa mapumziko ya muda ili kushughulikia mambo yake binafsi.

Maxime aliondolewa kwenye benchi la ufundi la Kagera Sugar Machi 6, mwaka huu kutokana na mwenendo mbaya wa kikosi hicho, ambacho hakijapata ushindi kwenye michezo nane mfululizo iliyopita, wakipoteza michezo minne na kutoa sare nne.

Akizungumzia mipango yake, Maxime amesema: “Baada ya kuachana na Kagera Sugar hivi karibuni, kwa sasa nimeamua kuwekeza nguvu zangu katika kufanya shughuli zangu binafsi, ambazo nilikuwa sipati nafasi ya kutosha kuzikamilisha kutokana na majukumu ya ukocha.

“Sijapata ofa yoyote ya kufundisha, na pia sipo tayari kwa sasa, kwa kuwa nataka kupata muda wa kupumzika na kukamilisha mambo yangu mengine na nitakapokamilisha hapo ndipo nitafikiria kuhusu masuala ya ofa.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YATAJA SABABU YA KUPIGWA 5G