Home Ligi Kuu KIPA MRUNDI ANAYEPIGIWA HESABU NA SIMBA AFIKIRIA KUWA WA KIMATAIFA

KIPA MRUNDI ANAYEPIGIWA HESABU NA SIMBA AFIKIRIA KUWA WA KIMATAIFA


JONATHAN Nahimana, kipa wa Klabu ya Namungo FC ambapo yupo huko kwa mkopo amesema kuwa hesabu zake kubwa ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kwa kuwa nafasi hiyo inawezekana kwa sasa kutokana na timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa.

Namungo ipo kwenye Kombe la Shirikisho ikiwa imetinga hatua ya mtoano ambapo ikifanikiwa kupenya mchezo wake dhidi ya Waangola itatinga hatua ya makundi.

Kipa huyo raia wa Burundi alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Simba kwenye usajili wa dirisha dogo ila mambo yalibuma baada ya Beno Kakolanya kuonyesha kiwango kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo aliifikisha timu hiyo hatua ya fainali.

Nyota huyo amesema:”Kupitia mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho nina amini kwamba itafungua njia ya mimi kucheza nje ya Bongo na kufanya niwe wa kimataifa.

“Nina amini kwamba kila kitu kinawezekana na hilo lipo wazi kwa kuwa tunafuatiliwa na wengi na hilo litafungua njia ya mimi kuwa kipa wa kimataifa,’ .

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA MWADUI FC