Home Namungo FC WAKATI SIMBA WAKIJIULIZA BAADA YA KIPIGO…’JULIO’ AIBUKA NA HILI…ATAMBA KUTIBUA ZAIDI MSIMBAZI…

WAKATI SIMBA WAKIJIULIZA BAADA YA KIPIGO…’JULIO’ AIBUKA NA HILI…ATAMBA KUTIBUA ZAIDI MSIMBAZI…


KOCHA Msaidizi wa Namungo FC, Jamhuri Kiwehlo ‘Julio’ amesema kuwa timu yao ina nafasi kubwa ya kuwapokonya Simba ubingwa wa ligi kuu msimu na huo ndiyo mpango wao.

Julio alifunguka kuwa anasema hivyo kwa kuwa ana kikosi na timu bora yenye uwezo wa kufanya lolote mbele ya timu yoyote kwenye ligi na ndiyo maana malengo yao msimu huu ni kuwa mabingwa.

Akizungumza na gazeti la Championi Jumatatu, Julio amesema Namungo ni moja kati ya timu bora na inayotoa ushindani wa kweli kwenye na ina uwezo wa kuchukua ushindi mbele ya Simba, Yanga, Azam na kila timu na hatimaye kuchukua ubingwa.

“Malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa msimu huu na uwezo wa kuchukua tunao. Namungo ni moja kati ya timu bora sana hapa Tanzania na inawezekana kuchukua pointi tatu kila uwanja.

“Namungo inaweza kuwafunga Simba, Yanga, Azam na kila timu, hakuna ambacho kinashindikana na ninasema kuwa Namungo atakuwa bingwa na hakuna atakayebisha,” alisema Julio.

Honour Janza kutoka Zambia alitambulishwa na uongozi wa Namungo kuwa kocha mkuu wa akisaidiwa na Julio na waliisimamia timu hiyo kwenye Mapinduzi na kuondoshwa hatua ya nusu fainali. Julio awatumia salamu Simba

SOMA NA HII  SAKATA LA YANGA KUNG'OA VITI JAMBO LINAMALIZWA HIVI WIZARA YATOA TAMKO