Home Habari za michezo WAKATI YANGA WAKIWAZA DABI…MO DEWJI AENDELEA KUTANGAZA NEEMA MPYA SIMBA…

WAKATI YANGA WAKIWAZA DABI…MO DEWJI AENDELEA KUTANGAZA NEEMA MPYA SIMBA…

Mwekezaji na Rais wa heshima wa klabu ya Simba Mo Dewji bado ameendelea kuiota ndoto ya kuiona klabu ya Simba ikibeba Ubingwa wa Afrika siku moja baada ya kufanya uwekezaji klabuni hapo.

Klabu ya Simba imekua ikifika hatua ya makundi na robo fainali kwa mara kadhaa sasa kutokana na uwekezaji alioufanya Mo dewji klabuni hapo kwa kipindi cha misimu isiyopungua mitano mpaka sasa.

Simba imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali mara mbili kwenye ligi ya mabingwa Afrika huku ikifika robo fainali moja kwenye kombe la shirikisho Afrika hii inaonesha ni kwa namna gani klabu ya Simba imejiimarisha kwenye michuano hiyo.

“Tulianza kwa kuchechemea kwenye michuano hii, Tulianza tukiwa wadogo sasa ni wakubwa na tunashindana na wakubwa wenzetu. Tunatakiwa kujipanga zaidi ili kwenda kuonyesha ubora bado naamini Simba itatwaa ubingwa wa Afrika siku moja” Alisema Mo Dewji.

Bilionea huyo ambaye ni mwekezaji ndani ya klabu hiyo amepanga amekua akiota klabu hiyo kufanya makubwa zaidi katika soka barani Afrika na hiyo ni kutokana na uwekezaji anaoufanya klabuni hapo.

SOMA NA HII  AZAM FC HAKUNA KUPOTEZA MUDA..MAMBO NI 'MPERA MPERA'..MWENDO WA KIJESHI...