Home Habari za michezo MOLOKO, AUCHO NA NGUSHI WARUDISHA ‘UTUKUFU’ YANGA…WAANZA UPYA KWA KASI YA ‘KIMONDO’…

MOLOKO, AUCHO NA NGUSHI WARUDISHA ‘UTUKUFU’ YANGA…WAANZA UPYA KWA KASI YA ‘KIMONDO’…


Benchi la ufundi la Yanga limefurahishwa na kurejea kwa haraka kwa winga wake Jesus Moloko na nyota wengine waliokuwa majeruhi likiamini watakuwa msaada mkubwa katika mechi zilizosalia za Ligi Kuu msimu huu.

Moloko aliyefanyiwa upasuaji wa goti mwanzoni mwa mwezi huu ameanza mazoezi mepesi baada ya kupona jeraha akiungana na Khalid Aucho na Crispin Ngushi ambao walikosekana kwenye baadhi ya michezo kutokana na majeraha.

Moloko alishuhudiwa akifanya mazoezi binafsi ya kukimbia katika Viwanja vya Gymkhana jijiji, juzi jioni chini ya usimamizi wa kocha wa viungo, Helmy Guedlich kwa takribani nusu saa.

Nyota huyo kutoka DR Congo alikuwa akikimbia taratibu kuzunguka uwanja ingawa alikuwa akipumzika kila alipotimiza mizunguko mitatu na baada ya kumaliza aliondoka viwanjani hapo.

Lakini wakati Moloko akianza mazoezi mepesi, daktari wa viungo, Youssef Mohamed amethibitisha kuwa Aucho na Ngushi wataungana na kikosi wiki ijayo kwa mazoezi ya pamoja.

“Aucho na Ngushi wameanza mazoezi ila bado wiki moja kuweza kufanya mazoezi na wenzao. Moloko bado yupo kwenye programu ya awali ya kujenga ufiti,” alisema Youusef.

Kurejea kwa nyota hao kumemkosha kocha Nasreddine Nabi aliyesema wataongezea nguvu zaidi katika harakati za kuwania ubingwa.

Nabi alisema kurejea kwa Ngushi ndio jambo kubwa zaidi lililomkosha kutokana na uhaba wa wachezaji wanaocheza nafasi ya mshambuliaji wa kati ambapo sasa kuna wawili wanaotumika kama chaguo la nafasi hiyo kina Fiston Mayele na Heritier Makambo.

“Nimefurahishwa na kurejea kwa wachezaji wangu waliokuwa majeruhi katika kipindi hiki ambacho tuna mechi nyingi ngumu na ushindani wa ligi umeongezeka kwani unaongeza wigo katika upangaji wa kikosi,” alisema Nabi.

“Kama Ngushi atarejea mapema itaongeza wigo katika nafasi ya mshambuliuaji wa kati. Kwa sasa wapo wawili Mayele na Makambo hivyo urejeo wa Ngushi ni jambo zuri kwetu.”

Timu hiyo inakabiliwa na mechi mbili ngumu zinazofuata kwenye Ligi Kuu ambazo ni dhidi ya Azam FC na Simba zinazofuata kwenye msimamo wa ligi na bila shaka urejeo wa Aucho na Ngushi utaongeza upana wa kikosi kuelekea mechi hasa ya Simba itakayochezwa Aprili 30.

SOMA NA HII  ODDS ZA UHAKIKA LEO ZIMELALA KWENYE MECHI HIZI....MKEKA WAKO USOME NA MERIDIANBET..

Yanga inaongoza ligi ikiwa imekusanya pointi 48 katika mechi 19 ilizocheza hadi sasa na inahitaji kupata ushindi katika mechi sita nane tu ili ijihakikishie ubingwa.