Home Habari za michezo KUHUSU MECHI ZA SIMBA NA YANGA…NABI KAVUTA HISIA WEEE..KISHA KWA UPOLE KASEMA...

KUHUSU MECHI ZA SIMBA NA YANGA…NABI KAVUTA HISIA WEEE..KISHA KWA UPOLE KASEMA HAYA..


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema ana dakika 180 za jasho na damu dhidi ya Azam FC na Simba ambazo anaamini ndizo zitakazompa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, msimu huu.

Lakini amewataka mastaa wake kujitoa kwa asilimia 90 na ana mpango wa kuongeza dozi kambini kwa mastaa kuelekea michezo hiyo miwili huku akiomba wachezaji wake watano walioitwa Taifa Stars kupambana ili kuendana na kasi ya wenzao na waingie kwenye kikosi cha kwanza.

Yanga ambao ni vinara kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, watakuwa wageni wa matajiri wa jiji la Dar es Salaam, Azam FC, mchezo utakaochezwa Aprili 6 mwaka huu.

“Nina mechi mbili ngumu ambazo zote zina dakika 180 za jasho na damu nahitaji kutwaa taji naamini kujitoa na ubora wa wachezaji wangu ndio itakuwa chachu ya mafanikio yangu hasa kwenye michezo yote miwili tataka pointi zote dhidi ya Azam FC na Simba,” alisema.

“Natamani kuwanoa wachezaji wangu wote kipindi hiki cha mapumziko kupisha michezo ya kirafiki kwa timu za taifa, lakini hilo litaniwia vigumu kutokana na baadhi yao kuitwa timu zao za taifa. Hao walioitwa wapate nafasi ya kucheza ili kujiweka fiti zaidi na kuendana na kasi ya wenzao.”

Nabi alisema hahitaji kuwa na mchezaji tegemezi kikosini anatamani kuona kila mmoja anawajibika kwa lengo la kuipambania timu iweze kufikia mafanikio.

SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO DABI..."GARI LA SIMBA LIMEWAKA "....UONGOZI WAWEKA MEZANI BILIONI 1 'CASH'....