Home Habari za michezo BAADA YA KUONA USHINDI ANAPATA KWA TABU…MGUNDA AANZA ‘KUGUNA’ NA SIMBA YAKE..

BAADA YA KUONA USHINDI ANAPATA KWA TABU…MGUNDA AANZA ‘KUGUNA’ NA SIMBA YAKE..

Habari za Simba

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amesema hana budi kuanza kuisuka upya safu yake ya Ushambuliaji, ili irejee katika hali yake ya kawaida baada ya kusuasua kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba SC ilipata wakati mgumu ilipocheza ugenini Singida dhidi ya wenyeji wao Singida Big Stars na kuambulia sare ya 1-1, kisha ikashinda kwa mbinde dhidi ya Ihefu FC nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars, Phiri alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 7, 20, 44, 52 na 71 huku Kibu Dennis akikosa nafasi ya kufunga dakika ya 47, 51 na 66.

Mgunda amesema kuwa furaha ya Kocha ni kuona timu inapata matokeo mazuri ambayo ni ushindi pale inapokuwa tofauti huwa hakuna anayefurahia jambo hilo.

“Kweli wachezaji wanapambana kusaka ushindi na wanacheza pia tunatengeneza nafasi nyingi lakini ambazo tunatumia ni chache hivyo hilo tunalifanyia kazi kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi zetu zote katika eneo la mazoezi,” amesema.

Safu ya ushambuliaji imetupia mabao 19 na kinara ni Moses Phiri mwenye mabao matano na pasi mbili za mabao.

Simba SC imeshajikusanyia alama 21 baada ya kucheza michezo 10, huku Young Africans ikiwa kileleni kwa kufikisha alama 23 baada ya kucheza michezo 9.

SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOSAFIRI KUELEKEA BOTSWANA