Home Habari za michezo SIMBA KUKIPIGA MECHI YA KIRAFIKI NA WALIOWAHI KUWAFUNGA GOLI 5….NGOMA ITACHEZWA CAIRO...

SIMBA KUKIPIGA MECHI YA KIRAFIKI NA WALIOWAHI KUWAFUNGA GOLI 5….NGOMA ITACHEZWA CAIRO KWENYEWE KULEEE…


Klabu ya Simba SC kesho Jumatano (Julai 27) itacheza mchezo mwingine wa Kimataifa wa Kirafiki ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika.

Simba SC imethibitisha taarifa za kutarajiwa kucheza mchezo huo wa Kirafiki kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ambapo imekua njia sahihi ya kuwafikishia ujumbe Mashabiki na Wanachama wake.

Taarifa iliyoandikwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Simba SC imeeleza kuwa kesho Jumatano kikosi cha Msimbazi kitacheza dhidi ya Haras El Hodoud ambao wanahistoria ya kuifunga Simba goli 5 kwenye mashindani ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo umepangwa kucheza mjini Cairo, ambapo kikosi cha Simba SC kitalazimika kusafiri kutoka mjini Ismailia kilipoweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/23.

“Kesho Jumatano tutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Haras El Hodoud ambao utapigwa jijini Cairo” imeeleza taarifa ya Simba SC

Simba SC imeshacheza michezo miwili ya Kirafiki tangu ilipoanza kambi nchini Misri majuma mawili yaliyopita, mchezo wa kwanza walikipiga Ismailia FC wakaambulia sare ya 1-1 kisha wakacheza dhidi ya Abou Hamad waliokubali kufungwa 6-0.

SOMA NA HII  KISA USAJILIWA BALEKE....MOSES PHIRI AANIKA WASIWASI WAKE SIMBA...AFUNGUKA A-Z...