Home Uncategorized AZAM FC YAIANDALIA DOZI MBAO

AZAM FC YAIANDALIA DOZI MBAO


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa unajiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Juni 14.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria alisema kuwa mipango ipo sawa kutokana na kikosi kuanza kurejea kwenye ubora wake.
“Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ameshaanza kukinoa kikosi na wachezaji wameanza kurejea kwenye utimamu wa mwili kwani walianza mazoezi ya pamoja tangu Mei 27, kilichobaki ni kutoa burudani kwa mashabiki.
“Kikubwa ni kwamba kila mchezaji kwa sasa anatambua majukumu yake ndani ya uwanja, hivyo tunaamini kwamba tutauzindua uwanja wetu rasmi kwa kubeba pointi tatu mbele ya Mbao FC,” alisema Zakazi.
Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 28 itamenyana na Mbao FC iliyo nafasi ya 19 na pointi zake 23 baada ya kucheza mechi 29.
SOMA NA HII  MSUVA AMFUATA SAMATTA ULAYA