Home Habari za michezo BAADA YA KUFUNGA ‘TUGOLI TUMOJA’ CHIRWA NAYE AANZA TAMBO ZA UFUNGAJI BORA...

BAADA YA KUFUNGA ‘TUGOLI TUMOJA’ CHIRWA NAYE AANZA TAMBO ZA UFUNGAJI BORA ETI…

Mshambuliaji wa Ihefu, Obrey Chirwa amesema ushindi wa mabao 2-1 walioupata dhidi ya Dodoma Jiji umeongeza morali na kwamba kazi ndio imeanza, huku akizungumzia bao na pasi aliyotoa kwenye ushindi huo havimvimbishi kichwa.

Ihefu imeshinda mchezo mmoja tu kati ya saba waliyocheza ikitoka sare mbili na kufungwa mechi nne imepanda hadi nafasi ya 14 kutoka kuburuza mkia ikiiacha Polisi iliyokuwa uwanja jana jijini Mbeya kuvaana na Namungo na Chirwa alisema ushindi huo wa kwanza kwao msimu huu ni mwanzo mzuri.

“Nimefungua akaunti ya mabao ni nzuri kwangu kwani bao langu limechangia timu kupata pointi tatu za kwanza lakini siwezi kufurahia bao hilo moja wakati timu imekosa matokeo kwenye mechi sita zilizopita sio afya kwetu,” alisema Chirwa na kuongeza;

“Tuna kikosi kizuri sijui tunakwama wapi, ila naamini matokeo tuliyoyapata yatakuwa na mwendelezo mzuri kwetu kwani tumefahamu wapi tulikuwa tunakosea na nini tunatakiwa kuongeza ili kuweza kuendelea kuwa bora na timu shindani tunahitaji kuondoka nafasi tuliyopo na kupanda zaidi.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGWA NA WAIVORY JUZI..SIMBA WAONA ISIWE TABU..WAANDIKA BARUA CAF...