Home Azam FC ISHU YA ‘SOPU’ YAIPASUA KICHWA AZAM FC…WACHUKUA MAAMUZI HAYA MAGUMU…

ISHU YA ‘SOPU’ YAIPASUA KICHWA AZAM FC…WACHUKUA MAAMUZI HAYA MAGUMU…

Nyota wa Azam FC, Abdul Suleiman ‘Sopu’ atafanyiwa vipimo zaidi ili kujua undani wa jeraha la misuli ya paja ‘hamstring’ linalomsumbua.

Sopu alishindwa kuendelea na mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho dakika ya pili tu dhidi ya Al Akhdar kutoka Libya huku akishuhudia timu yake ikishindwa kutinga hatua ya makundi kufuatia kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 licha ya ushindi wa 2-0.

Akizungumza daktari wa kikosi hicho, Mwanandi Mwankemwa alisema ; “Tumempa siku tatu za kuendelea na matibabu na kama ataendelea hivi alivyo kwa sasa tutamfanyia kipimo cha MRI kwa ajili ya kugundua tatizo zaidi, hali yake sio mbaya sana ingawa hawezi kucheza kwenye michezo yetu ya karibuni.”

Kwa upande wa Sopu alisema licha ya kutoonyesha kiwango chake kilichotarajiwa na mashabiki zake hadi sasa ila bado ana nafasi ya kuendeleza kile alichokionyesha wakati akikitumikia kikosi cha Coastal Union kwa msimu uliopita alipoonekana.

SOMA NA HII  KISA KIPIGO TOKA AZAM FC....MGUNDA KAWAKA KINOMA HUKO SIMBA...HATAKI SAMAHANI....