Home news KISA YANGA …MWENYEKITI SIMBA ACHACHAMAA…. AIBUKA NA JAMBO JIPYA HUKO..

KISA YANGA …MWENYEKITI SIMBA ACHACHAMAA…. AIBUKA NA JAMBO JIPYA HUKO..


MWENYEKITI wa Simba, Murtaza Mangungu, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia wasiogope kasi ya wapinzani wao Yanga huku akiahidi kuubakisha ubingwa wa Ligi Kuu Bara Msimbazi.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuiona Yanga ikiwa kileleni ikiwa na pointi tisa, ikishinda michezo yake mitatu ya ligi katika msimu huu.

Simba yenyewe imecheza michezo miwili kati ya hiyo wametoka suluhu na Biashara United huku ikiwafunga Dodoma Jiji bao 1-0, lililofungwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere.

“Mechi tatu haziwezi kuwapa ubingwa au kututoa kwenye mbio za ubingwa. Ligi ni mbio ndefu na sisi Simba ubingwa wetu uko palepale.

“Wanasimba waondoe hofu, tupo vizuri kama viongozi katika utendaji, pia benchi la ufundi linaloendelea kufanya maandalizi ya kikosi chao,” alisema Mangungu.

SOMA NA HII  HASSAN DILUNGA HATARINI SIMBA...MUDA WOWOTE ANAWEZA KUONDOKA