Home Habari za michezo KUHUSU LOMALISA KUSEPA ZAKE YANGA…UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA…

KUHUSU LOMALISA KUSEPA ZAKE YANGA…UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA…

Habari za Yanga SC

Beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa Mutambala huenda akaachwa na klabu yake hiyo kutokana na kupata majeraha ya mara kwa mara yanayomuweka nje wa uwanja Kwa muda mrefu.

Beki huyo maarufu kama waziri wa maji amekuwa akikosekana katika mechi muhimu za kikosi hicho kutokana na majeraha hayo jambo ambalo limesababisha uongozi wa klabu hiyo kutoharakisha mazungumzo ya mkataba mpya baada ya ule alionayo kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa klabu hiyo imeamua kutomuongezea mkataba beki huyo ili kutafuta mbadala wake atakayekuwa anapatikana muda mwingi kusaidia kikosi hicho.

Jambo hilo limechagiza uongozi wa Yanga kuona ni bora kumpa mkataba wa kudumu beki Nickson Kibabage ambaye yupo kwa mkopo katika klabu hiyo akitokea Singida Fountain Gate na kuamua kumpa mkataba wa miaka mitatu baada ya mazungumzo na Singida Fountain Gate kukamilika.

Lomalisa Mutambala amekuwa na takwimu zisizoridhisha msimu huu akiwa ametoa asisti moja tu huku mshindani wake beki mzawa Kibabage akiwa na asisti 4 mpaka sasa.

Ripoti ya awali ya kocha Gamondi inahitaji beki wa pambeni mwenye kiwango kikubwa na aliye fiti muda mwingi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA AJIBU KAMA 'YUPO HAYUPO'...KOCHA MSOMALI WA AZAM KAONA ISIWE TABU..KAAMUA HILI..