Home Azam FC BAADA YA KUONA AJIBU KAMA ‘YUPO HAYUPO’…KOCHA MSOMALI WA AZAM KAONA ISIWE...

BAADA YA KUONA AJIBU KAMA ‘YUPO HAYUPO’…KOCHA MSOMALI WA AZAM KAONA ISIWE TABU..KAAMUA HILI..


KOCHA Mkuu wa Azam FC, Abdihamid Moallin amesema licha ya kikosi chake kuzidi kuimarika, lakini kwa sasa jukumu alilonalo ni kuhakikisha kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu anarejea kwenye makali yake.

Moallin alisema nyota huyo alianza vizuri baada ya kusajiliwa dirisha dogo la Januari akitokea Simba ila majeraha ya mara kwa mara yamemrudisha nyuma na kumfanya kumuondoa kwenye programu zake na sasa anaanza kumpika upya.

“Kila mtu anatambua uwezo wake na alionyesha kiwango kizuri wakati wa michuano ya Mapinduzi, ila kwa siku za hivi karibuni ameandamwa na majeraha hivyo nitahakikisha anarejesha makali yake,” alisema kocha huyo.

“Sababu za kumpa dakika chache za kucheza katika mchezo wetu wa kirafiki na DTB ni kwa ajili ya kumpa mechi fitinesi na ameonyesha kiwango kizuri kwani wapinzani tuliocheza nao ni wazuri na wana wachezaji bora.”

Ajibu alicheza mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, ambapo Azam ilishinda kwa bao 1-0, lililofungwa na Edward Manyama na huenda akawa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachovaana na Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara utakaochezwa Aprili 6 jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  SAA KADHAA KABLA YA KUKIPIGA NA MAZEMBE....FEI TOTO NA MORRISON WAACHA MSALA YANGA..