Home Habari za michezo 🚨TUSIMAMIE SHERIA,TUACHE UBABAISHAJI! YANGA SC IPOKONYWE POINT BILA KUANGALIA USONI!

🚨TUSIMAMIE SHERIA,TUACHE UBABAISHAJI! YANGA SC IPOKONYWE POINT BILA KUANGALIA USONI!

Habari za Yanga leo

Kuna ukimya wenye harufu mbaya baada ya @fifa kuifungia Klabu ya @yangasc kufuatia kushindwa kumsajili mmoja wa wachezaji wake muhimu waliyemtumia katika ligi. Baada ya FIFA kuifungia Yanga, @tanfootball nao wakachukua jukumu kwa shingo upande kuifungia Yanga.

Turudi kwenye sheria za FiFa na kanuni za mpira ni kwamba mchezaji asiposajiliwa rasmi kwenye mifumo yote ya fifa na tff basi mchezaji huyo ni batili. Hivyo kimantiki mchezaji huyo ambaye hakutimiza masharti ya usajili kamili ni BATILI na kama alicheza katika ligi yetu basi michezo husika itahesabika ni batili na hivyo klabu yake itapoteza michezo husika, Yanga inatakiwa kupokwa pointi 3 na magoli mawili kwa kila mchezo ambao mchezaji husika anayetajwa na fifa kuwa hakutimiza masharti ya usajili alicheza!

TFF inashiriki uharamia, kitendo tu cha kuficha jina la mchezaji husika kinadhihirisha hila waliyo nayo TFF dhidi ya tendo hili ambalo Yanga wanatakiwa kuwajibika kwa uzembe wao.

Tusimamie sheria, tuache ubabaishaji! Yanga ipokonywe point bila kuangaliana usoni!

Habari hii imekopiwa kutoka kwa mwanamichezo/mwanaharakati  maarufu nchiniYericko nyerere ambapo aliandika kwenye ukurasa wake wa X.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTOPEWA NAFASI...MUKOKO SHINDWA KUJIZUIA YANGA...AFUNGUKA ANAYOPITIA...