Home news BAADA YA KUTOPEWA NAFASI…MUKOKO SHINDWA KUJIZUIA YANGA…AFUNGUKA ANAYOPITIA…

BAADA YA KUTOPEWA NAFASI…MUKOKO SHINDWA KUJIZUIA YANGA…AFUNGUKA ANAYOPITIA…


KIUNGO nyota wa Yanga kwa msimu uliopita, Mukoko Tonombe ameweka wazi kuwa anapitia magumu ndani ya timu hiyo kwa sasa baada ya kutokuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza.

Tonombe aliweka wazi hilo baada ya kuandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao ulionyesha kutokuwa na hali nzuri baada ya nafasi yake ya kucheza kuwa finyu.

Ujumbe wa Mukoko ulikuwa wa pande tatu, moja kuwashukuru Watanzania na Wanayanga kwa kumsapoti toka amefika nchini, ujumbe mwingine ulihusu nia yake ya kutaka kufanikiwa akiwa Yanga na mwingine ukionyesha matumaini ya kuyashinda majaribu.

Tonombe aliandika: “Asante sana Mungu wangu kwani umefanikisha ndoto yangu hapa Tanzania kuja kunipa vikombe vyote.

“Asante sana shabiki wangu wa Yanga natumai bado hata maisha yamekuwa magumu ila nitafanikiwa. Naamini na namshukuru Mungu sana.”

Mukoko kwa sasa anakabiliwa na ushindani wa namba baada ya timu hiyo kuwasajili viungo Khalid Aucho na Yannick Bangala.

SOMA NA HII  HAWA SIMBA, YANGA MBONA KAMA WANATULETEA UTANI KIMATAIFA