Home news FT: SIMBA 2-1 AZAM FC…..KANOUTE ALIAMSHA …SAKHO AWAVURUGA…VARANE ACHAPWA KOFI…

FT: SIMBA 2-1 AZAM FC…..KANOUTE ALIAMSHA …SAKHO AWAVURUGA…VARANE ACHAPWA KOFI…


DAKIKA 90, zimemalizika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ‘Dabi ya Mzizima’ kati ya Simba na Azam FC kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam kufanya mabadiliko baada ya kumtoa Charles Zulu na nafasi yake kuchukuliwa na Tepsie Evance.

Mabadiliko hayo yalionekana kuleta tija kwa upande wa Azam ambao walikuwa wanategemea mashambulizi ya kushitukiza kupitia kwa Tepsie Evance na Ismail Aziz Kader.

Dakika ya 58, Azam iliendelea kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Mudathir Yahaya, Idris Mbombo huku nafasi zao zikichukuliwa na Shaban Iddy Chilunda na Rodgers Kola.

Dakika 66, Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Meddie Kagere, Larry Bwalya huku nafasi zao zikichukuliwa na Mzamiru Yassin na Chris Mugalu.

Dakika ya 67, Simba ilipata bao la utangulizi kupitia kwa Sadio Kanoute aliyepiga kichwa safi baada ya Friikiki iliyopigwa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’

Simba ilipata bao la pili dakika ya 72, kupitia kwa Pape Ousmane Sakho baada ya mabeki wa Azam Daniel Amoah na Abdallah Kheri kumsindikiza kwa macho kufuatia pasi safi iliyopigwa na Kibu Denis.

Azam ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Rodgers Kola dakika ya 80, kufuatia krosi iliyopigwa na Tepsie Evance.

Aidha katika hali isiyo ya kawaida, Enock Inonga ‘Varane’ alijikuta kwenye wakati mgumu, mara baada ya kuchapwa kofi na mshambuliaji wa Azam Idrisa Mbombo.

Tukio hilo halikuweza kuona na mwamuzi wa mchezo huo, hivyo mtendaji hakuadhibiwa .

Katika michezo 11, iliyopita ambapo timu hizo zimekutana Simba imeshinda sita, sare nne, huku Azam FC ikishinda mchezo mmoja tu.

Huu ni mchezo wa 27, kwa timu hizi kukutana kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ambapo Azam imeshinda mitano, sare tisa na kupoteza 13.

Matokeo haya yanaifanya Simba kufikisha pointi 24, ikiwa nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 29, baada ya michezo 10, wakati Azam FC inashika nafasi ya saba na pointi 15, baada ya kucheza michezo 11.

SOMA NA HII  MNAWASIFIA SANA MAMELODI SUNDOWNS...WATAPIGWA NA SIMBA MSHANGAE