Home news MORRISON ‘BANA’…WAKATI WENZAKE WAKIENDELA KUPAMBANA ..YEYE YUKO KWAO AKIFANYA ‘PATI’…

MORRISON ‘BANA’…WAKATI WENZAKE WAKIENDELA KUPAMBANA ..YEYE YUKO KWAO AKIFANYA ‘PATI’…

 


WAKATI Simba ikiwa mkoani Tabora tangu jana ikijifua tayari kuwavaa KMC leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, winga wake Benard Morrison jana alikuwa na jambo lake.

Mchezaji Bora wa Simba kwa mwezi uliopita, yupo kwao Ghana kwa mapumziko maalumu na jana alikuwa na jambo lake la kurudisha shukrani kwa kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji.

Taarifa kutoka Ghana zinasema, Morrison akishirikiana na faimilia yake waliandaa jambo hilo na kuliita ‘BM3fFamily Soccer Fest’, huku likifanyika kwenye viwanja vya Effia Police Park.

Vyakula, mavazi, vifaa vya michezo na mahitaji mengine ya muhimu katika jamii hiyo vilitolewa na Morrison ambaye amekuwa mhimili wa ndani ya Simba kwa msimu huu, akiisaidia kwenye mechi za ligi na zile za Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  KISA KIPIGO CHA GOLI 5 BILA KUTOKA SIMBA....KOTEI AIBUKA NA HAYA MAPYA MTIBWA SUGAR...