Home Uncategorized MENEJA WA KIUNGO WA PLATEU UNITED ANAYEWINDWA NA YANGA AFUNGUKIA DILI HILO

MENEJA WA KIUNGO WA PLATEU UNITED ANAYEWINDWA NA YANGA AFUNGUKIA DILI HILO


MENEJA wa nyota wa Plateau United, Isah Ndala amesema kuwa mchezaji huyo ana ofa nyingi kutoka timu mbalimbali ambazo zinahitaji kupata saini yake ikiwa ni pamoja na Yanga.

Ibrahim Ahmed ambaye ni meneja amesema kuwa mchezaji wake amekuwa akiwaniwa na timu nyingi kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja.


Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuwania saini yake ni pamoja na Yanga ambao walivutiwa na uwezo wake baada ya kucheza na Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.


Ahmed amesema:”Zipo timu nyingi ambazo zinaiwania saini ya mchezaji Ndala kwa sababu ana uwezo mkubwa na anajiamini hivyo nina amini kwamba ikiwa kuna timu itapata saini yake basi itapata faida kubwa.


“Kwa Tanzania zipo timu ambazo tumeanza mazungumzo nazo ikiwa ni pamoja na Yanga ila siwezi kusema kwamba kwa sasa tumefikia wapi na nini kiandelea kwa kuwa ni siri,” .


SOMA NA HII  DAVIES ATAJA SABABU YA KUENDELEA KUBAKI BAYERN MUNICH