Home Habari za michezo HUKU AZIZ KI, KULE FEI TOTO…MTASEMA WENYEWE NANI BORA

HUKU AZIZ KI, KULE FEI TOTO…MTASEMA WENYEWE NANI BORA

habari za yanga-fei toto

MSIMU mpya wa Ligi kuu unarudi tena kuanzia Agosti 16 ambapo ile vita kati ya Aziz Ki na Fei Toto imerejea tena.

Katika mchezo wa leo Fainali ya Ngao ya Jamii, mastaa hawa ambao wamewahi kucheza pamoja wakiwa Yanga, watakutana na kuoneshana tena umwamba.

Kulikuwa na ushindani mkubwa msimu uliopita baina ya Stephane Aziz Ki na Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambao mwishoni Aziz Ki aliibuka mshindi.

Nyota huyo wa Yanga kutoka Burkina Faso alimuacha kwenye mataa Fei Toto kwa kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu na kisha kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi kisha kuchukua tuzo ya kiungo bora wa ligi.

Ushindani wao unaonekana unarudi upya msimu huu kutokana na kile ambacho wamekifanya kwenye mechi za hivi karibuni za timu zao.

Fei Toto amefunga mabao matatu katika mechi sita zilizopita za Azam kama ilivyo kwa Aziz Ki ambaye amefunga idadi hiyo ya mabao kwa Yanga katika mechi tano zilizopita.

SOMA NA HII  NDONDO CUP MARUFUKU..."HATUJATOA KIBALI CHOCHOTE" TFF