Home Geita Gold FC BALAA JINGINE LEO…SIMBA NA COASTAL KUMALIZANA UWANJANI

BALAA JINGINE LEO…SIMBA NA COASTAL KUMALIZANA UWANJANI

habariza simba na yanga

KUNA Mambo mawili yanaweza kuifanya mechi kati ya Simba na Coastal ya kuwania mshindi wa tatu ikawa na mvuto na ushindani wa aina yake.

Kwanza ni hamu ya kupoza machungu kwa kila upande baada ya kushindwa kutinga fainali ya Ngao ya Jamii na hivyo kupoteza fursa ya kushinda taji la kwanza msimu huu.

Lakini la pili ambalo ni kubwa zaidi ni hamu ya kulipa kisasi ambayo kila moja itakuwa nayo kwa mwenzake kutokana na sababu tofauti.

Simba ina hasira ya kupokonywa mchezaji Lameck Lawi ambaye ilimsajili kutoka Coastal, lakini katika hali ya kushangaza, timu hiyo ya Tanga ilibadilisha uamuzi ghafla na kurudisha fedha ilizopewa katika mauzo ya mchezaji huyo na kumuuza Ubelgiji katika timu ya KAA Gent.

Coastal yenyewe bila shaka inataka kulipa kisasi cha kupoteza mechi mbili za ligi msimu uliopita dhidi ya Simba ikifungwa mabao 3-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza ugenini na kisha ikapoteza kwa mabao 2-1 nyumbani.

SOMA NA HII  ALI KAMWE...HATUJAZOEA GOLI MOJA...TUNA TIMU BORA