Home Habari za michezo MKUDE APOTEA SIMBA….MARA YA MWISHO KUONEKANA ALIKUWA DUBAI…ISHU NZIMA IKO HIVI…

MKUDE APOTEA SIMBA….MARA YA MWISHO KUONEKANA ALIKUWA DUBAI…ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Simba leo

Pamoja na Jonas Mkude kutoonekana kwenye kikosi cha kwanza cha Simba kwa dakika 550 amekingiwa kifua na mastaa wa zamani wa timu hiyo wakidai bado ana uwezo wa kuisaidia timu huko mbele.

Mkude hajawa sehemu ya kikosi cha Simba hivi karibuni licha ya kupona majeraha yake na mara ya mwisho kuwa sehemu ya timu hiyo ni katika mechi za kirafiki dhidi ya CSK Moscow nchini Dubai akiwa amekaa kwenye benchi.

Baada ya hapo Mkude hajacheza mechi dhidi ya Mbeya City, Dodoma, Singida zikiwa ni za Ligi Kuu Bara, akakosa FA dhidi ya Coastal na mechi ya kirafiki dhidi ya Al Hilal iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa pamoja na mechi ya juzi dhidi ya Horoya.

Inafahamika kuwa kiungo huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichokuwa kwenye mazoezi yanayoendelea katika uwanja wa Mo Simba Arena lakini kwenye mechi akawa haonekani pamoja na kuwa yeye ndiye mzoefu zaidi kwenye timu hiyo.

Mshambuliaji wa zamani Simba, Bakari Kigodeko alisema Mkude ni mchezaji mzuri hivyo anaweza kurejea kwenye ubora wake kama ilivyokuwa zamani.

Kigodeko alisema inawezekana kutoka kwenye kikosi cha kwanza basi kisaikolojia hayupo sawa lakini kama akitulia kila kitu kitarudi kama zamani.

“Mkude alikuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza lakini kadri siku zilivyokuwa zinaenda mbele alijikuta akikaa benchi na kutoonekana kabisa zamani yeye alikuwa anaanza na Mzamiru (Yassin) anakuwa benchi lakini kwa sasa ni tofauti,” alisema Kigodeko.

Upande wa beki wa zamani Simba, Fikiri Magoso alisema yeye anampa heshima kubwa Mkude kwa sababu ameifanyia makubwa Simba hadi kufika ilipo.

“Kuna wakati hata Mzamiru alikuwa benchi na Mkude akawa anaanza na sasa upepo umegeuka lakini kwenye mpira ni mambo ya kawaida sana kwa sababu unaweza kubadilisha na wewe muda wowote,”alisema Magoso.

Mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakiletewa mbadala kila mwaka ili kumuongezea ushindani lakini msimu huu anaonekana kucheza kwa dakika chache zaidi ingawa wadau wanadhani kwamba bado Mkude yuko kwenye ubora wake na punde atarejea kwa nguvu kubwa.

SOMA NA HII  SARE YA SIMBA vs AL AHLY YAMUIBUA MSIGWA AFUNGUKA KUHUSU GOLI LA MAMA