Home Yanga SC LAMINE MORO AENGULIWA KIKOSI CHA YANGA

LAMINE MORO AENGULIWA KIKOSI CHA YANGA

 IMEELEZWA kuwa beki wa Yanga Lamine Moro ameondolewa kikosini kutokana na utovu wa nidhamu.

Kwa sasa kikosi cha Yanga kipo Lindi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa leo majira ya saa 10:00 jioni.

Alipotafutwa Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa ili azungumzie suala hilo alijibu kuwa yupo safarini.

Mtu wa karibu wa Lamine amesema kuwa nyota huyo kwa sasa hayupo sawa ila hajaweka wazi kinachomsumbua.

SOMA NA HII  SANKARA AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU YANGA