Home Habari za michezo NDONDO CUP MARUFUKU…”HATUJATOA KIBALI CHOCHOTE” TFF

NDONDO CUP MARUFUKU…”HATUJATOA KIBALI CHOCHOTE” TFF

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa likiwa ndio
mamlaka inayosimamia na kutoa vibali vya michezo ya soka nchini halijatoa kibali kwa ajili ya mashindano ya Ndondo Cup ambayo yametangazwa na Clouds Media.

Mashindano hayo yametangazwa rasmi leo Machi 22, 2023 na Mkurugenzi wa Mshindano hayo, Shaffih Kajuna maarufu kama Shaffih Dauda ambaye pia ni mtangazaji wa chombo hicho cha habari kupitia kipindi cha Clouds 360.

Ikumbukwe pia kuwa, Shaffih alifungiwa na Shirikisho hilo kujihusisha na masuala ya soka kwa miaka mitano.

SOMA NA HII  KISA KIPIGO CHA JANA DHIDI YA UGANDA....KOCHA TAIFA STARS ATOKOMEA GHAFLA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here