Home Uncategorized KUMEKUCHA SIMBA, MBELIGJI APEWA MECHI TATU AKIZINGUA MOJA KUPIGWA CHINI JUMLAJUMLA

KUMEKUCHA SIMBA, MBELIGJI APEWA MECHI TATU AKIZINGUA MOJA KUPIGWA CHINI JUMLAJUMLA

LICHA ya kuipa Simba ubingwa wa tatu mfululizo bado maisha yake ndani ya kikosi hicho hayana muda mrefu kutokana na mvutano uliopo ndani ya uongozi.

Habari zinaeleza kuwa kikubwa kitakachomponza Sven Vandenbroeck ni misimamo yake ya kufuata misingi ya ukocha jambo linalomfanya asiwe na kundi linalompa sapoti kwa sasa pamoja na mkataba kufika ukingoni.

Sven raia wa Ubelgiji alipokea mikoba kutoka kwa

Patric Aussems maarufu kama Uchebe ambaye naye kutolewa kwake kulisababishwa na misimamo yake licha ya kuwa na uwezo mkubwa ndani ya uwanja.

Uchebe alisepa baada ya kusimamishwa kwa muda na uongozi wa Simba ambao baadaye ulitoa taarifa kwamba Patrick amepigwa chini kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri ndani ya kikosi.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa:”Ishu ya kuzuia wachezaji kushangilia ubingwa walipotoka Lindi bado inaishi kwenye mioyo ya viongozi muda wowote kuanzia sasa anaweza kupigwa chini kinachosubiriwa ni sehemu ya kutokea tu.

“Mechi hizi tatu alizonazo mkononi ndizo zimeshikilia hatma yake, ile ya Mbao kupigwa mashabiki wanajua kikosi kilikuwa cha ushkaji sasa ipo yenyewe kubwa akiboronga tu safari imewadia,” kilieleza chanzo hicho.

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa afafanue kuhusu dili la Sven pamoja na mkataba wake alisema:”Siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo,”.

SOMA NA HII  INTER MILAN NA MANCHESTER UNITED ZINAKOMOANA ISHU YA LUKAKU