Home Uncategorized MESSI AMPOTEZA MAZIMA BENZEMA WA REAL MADRID

MESSI AMPOTEZA MAZIMA BENZEMA WA REAL MADRID


Mashine ya kazi ndani ya La Liga msimu wa 2019/20 ametupia mabao 25 na ametoa jumla ya pasi 21 zilizotengeneza mabao.

Lionel Messi amempoteza Karim Benzema wa Real Madrid ambao ni Mabingwa wa La Liga kwa idadi ya mabao manne.

Benzema ametupia mabao 21 na kutoa jumla ya pasi nane za mabao ndani ya La Liga. 

Messi ametumia jumla ya dakika 2,880 uwanjani akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 115.

Benzema ametumia jumla ya dakika 3,152 uwanjani akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 150.

SOMA NA HII  MANARA - UWEZO WETU NI KUSAJILI MCHEZAJI WA MILIONI 230 TU..!!