Home Uncategorized BREAKING:KABLA YA KUWAVAA SIMBA, AZAM FC YAMUONDOA KIONGOZI WAO MMOJA

BREAKING:KABLA YA KUWAVAA SIMBA, AZAM FC YAMUONDOA KIONGOZI WAO MMOJA


JAFFARY Maganga aliyekuwa Ofisa Habari wa Azam FC amebadilishiwa nafasi ya cheo chake.

Maganga ameondoka kwenye nafasi hiyo ikiwa imebaki siku moja kwa timu ya Azam FC kumenyana na Simba, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Machi 4, Uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maganga amesema kuwa kwa sasa hatokuwa Ofisa Habari wa Azam FC amebadilishiwa majukumu atabaki kuwa mwanafamilia wa Azam FC kwenye majukumu mengine.

“Leo, Machi 2, 2020 rasmi sitakuwa Ofisa Habari wa Azam FC kwani kampuni imenibadilishia majukumu na nitaendelea kuwa mwanafamilia wa Azam FC, naomba ushirikiano uendelee kuwepo kati ya huyo ambaye atakuja kwani sote ni ndugu,” amesema.

SOMA NA HII  HAO YANGA WANABALAA WAMCHAPA MTU NANE