Home Uncategorized MBAO FC WAO NI WABISHI KINOMA, CHEKI MAFANIKIO YAO NA HESABU

MBAO FC WAO NI WABISHI KINOMA, CHEKI MAFANIKIO YAO NA HESABU

MBAO FC wao wanajiita wabishi ni Klabu ambayo inapatikana kanda ya ziwa ikiwa chini Kocha Mkuu, Abulmutik Haji ambaye msimu wa 2018/19 alikuwa ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting.
Wakazi wa Mwanza wanajivunia timu yao ambayo imekuwa na mashabiki wengi kutokana na sera yake ya kujiita wabishi jambo linalowapa imani ya kuendelea kutusua ndani ya ligi licha ya kupitia kipindi kigumu kwa sasa.
Imeanzishwa mwaka 2005 na makao makuu yake makuu ni hukohuko kuliko na mawe mengi na utajiri wa ziwa Victoria Mwanza.
Uwanja wake
Klabu ya Mbao inatumia Uwanja wa CCM Kirumba wenye uwezo wa kubeba watu 35,000 kwa mechi kubwa na zenye ushindani mfano zile za Simba na Yanga ama iwapo itakuwa ni dabi yao dhidi ya Alliance FC na Uwanja wa  Nyamagana.
Kushiriki Ligi Kuu
Ilipanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17. Kocha wao msimu wa kwanza alikuwa ni Ettiene Ndayiragije ambaye raia wa Burundi.
Msimu huu wa 2019/20 ni msimu wake wanne ikiwa imecheza msimu wa 2016/17, 2017/18, 2018/19 na 2019/20 bila kushuka daraja.
Mafanikio
Iliweza kushiriki Fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka 2017. Mei 27 iliitoa jasho Simba kwenye fainali ya kibabe.Mchezo huo ulichezwa kwa muda wa dakika 120 baada ya dakika 90 kukamilika kwa timu zote bila kufungana.
Simba ilishinda mabao 2-1 usiku kabisa kwa penalti iliyopigwa na Shiza Kichuya ilikuwa Uwanja wa Jamhuri, makao makuu ya nchi Dodoma.
Januari 27/2019 ilishiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya SportPesa na ilimvua ubingwa bingwa mtetezi Gor Mahia ila iliishia nafasi ya nne kwa kufungwa na Simba kwa penalti 5-3 Uwanja wa Taifa.
Metacha Mnata aliibuka mlinda mlango bora wa mshindano hayo na hapo hesabu za Yanga kuiwinda saini yake zilianzia na alipoitwa timu ya Taifa ya Tanzania mipango ikajipa sasa ni mali ya Yanga.

Kosi lao la 2016/17
Benedict Haule, Boniphace Maganga, David Mwasa, Asante Kwasi, Yusuph Ndikumana, Salimin Hozza, Habibu Haji, Ibrahim Njohole, Pius Buswita, George Sangija, Jamal Mwambeleko,Mussa Mohamed, Alex Ntiri, Vincent Philipo, Ndaki Robert, Dickson Ambundo, Steve Mbaya na Rajesh Kotecha.
Baadhi ya makocha walioinoa Mbao
Ettiene Ndayiragije, Amri Said aliyebwaga manyanga baada ya kuletewa kocha msaidizi Ally Bushiri msimu wa 2018/19 baadaye alipigwa chini kutokana na mwenendo mbovu.Hemed Morroco alianza msimu wa 2019/20 akiwa sambamba na Abdulmutik Haji ila mambo yalipokuwa magumu walibwaga wote manyanga kabla ya Haji kurejea kwenye benchi la ufundi.
Kwa sasa ipo hapa
Wabishi wapo nafasi ya 19 baada ya kucheza mechi 29 wakiwa na pointi zao 23 na mabao 19 ya kufunga huku wakifungwa mabao 38.
Mipango yao
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njash ameliambia Championi Jumatano kuwa kwa sasa hawana mipango yoyote kila kitu kimesimama kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo linaitikisa dunia.
Mbao kwao ilikuwa njia
Dickson Ambundo kwa sasa anakipiga ndani ya Gor Mahia ya Kenya, Ndayiragije naye kwake ilikuwa njia kwani aliibukia KMC msimu wa 2018/19 kisha Azam FC na kwa sasa maisha yake yanaendelea ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Kwasi aliibukia Lipuli akaonekana na Simba ambayo alitinga nayo hatua ya robo Fainali ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19.
Mtambo wao wa mabao
Wazir Junior ndiye kinara wa utupiaji ndani ya Mbao ambapo amehusika kwenye mabao 9 kati ya 19. Amefunga mabao saba na kutengeneza pasi mbili za mabao.
Nyota huyo amesema kuwa wana imani iwapo ligi itarejea mechi zao zote zilizobaki watapambana mithili ya fainali kupata matokeo chanya yatakayowabakisha ndani ya ligi.
SOMA NA HII  MANULA AWABURUZA MGORE NA BAROLA, ASEPA NA TUZO YAKE