Home Habari za michezo KISA KIPIGO TOKA AZAM FC….MGUNDA KAWAKA KINOMA HUKO SIMBA…HATAKI SAMAHANI….

KISA KIPIGO TOKA AZAM FC….MGUNDA KAWAKA KINOMA HUKO SIMBA…HATAKI SAMAHANI….

Kocha Msaidizi Simba SC

Kocha wa muda wa Simba Sc, Juma Ramadhani Mgunda amesema kwamba hachukulii uchovu kama sababu ya kuwafanya wapoteze mchezo wao dhidi ya Azam FC.

Mgunda amesema kwani ratiba imepangwa ili wao kama timu waweze kuifuata na kuikamilisha licha ya uchovu uliopo kwa wachezaji wake kutokana na ratiba ngumu waliyokuwa nayo.

“Fatigue ina sehemu kubwa sana lazima nikiri hilo lakini kuna vitu vingine huwezi kusema, kwa sababu mchezo wa mpira umepangwa na ni lazima tucheze na ukiangalia ratiba yetu imebanana sana lakini siwezi kusema ndio sababu, anayejua mpira ataelewa ninachosema.

“Tumecheza na De Agosto, baada ya siku tano tukacheza dabi (Simba na Yanga), baada ya siku tatu tumecheza leo (Simba na Azam), Oktoba 30 tutacheza tena hapa Dar, Novemba 4 tutacheza tena, na Novemba 9 tutacheza tena Singida na Novemba 12 tutacheza tena hapa Dar.

“Kwa hiyo utaona ratiba ilivyo ngumu na sehemu ya fatigue ipo lakini sitaki kusema kama ndiyo sababu. Kwa sababu ratiba ipo lazima tutumikie kama ilivyopangwa ili tupate matokeo mazuri,” amesema Mgunda.

SOMA NA HII  ORODHA YA MASTAA TISA NDANI YA SIMBA AMBAO MIKATABA YAO ITAFIKA UKINGONI