Home Habari za michezo BAADA YA KUTINGA ROBO FAINAL…MESSI ‘AISNICHI’ UINGEREZA KWENYE MBIO ZA UBINGWA QATAR..

BAADA YA KUTINGA ROBO FAINAL…MESSI ‘AISNICHI’ UINGEREZA KWENYE MBIO ZA UBINGWA QATAR..

SUPASTAA Lionel Messi amezifanyia uchambuzi timu zilizobaki kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 kwa maana ya zile zenye uwezo wa kubeba ubingwa, lakini amewaweka kando England kwamba hawashawishi.

Messi alifunga bao la kwanza kwenye mechi ya raundi ya 16 bora ya fainali za Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Australia na hivyo kumfanya afikishe idadi ya mabao matatu katika mechi nne alizocheza huku akiwezesha Argentina kutinga hatua ya robo fainali ambapo watakipiga na Uholanzi.

Messi alifunga pia kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya makundi katika kichapo cha kushtua kutoka kwa Saudi Arabia na alifunga tena kwenye mechi ya pili dhidi ya Mexico, lakini hakutikisa nyavu kwenye mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi dhidi ya Poland.

Messi aliulizwa ni timu gani zilizobaki kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia 2022 anadhani inashawishi kwenye mbio za ubingwa. Fowadi huyo supastaa alizitaja timu tatu nje ya Argentina, lakini England hakuwaweka kabisa kwenye orodha hiyo akidai kwamba si miongoni mwa timu zinazomshawishi kwenye michuano hiyo ya Qatar.

“Tumeona mechi zote za Kombe la Dunia,” alisema Messi na kuongeza. “Brazil wanacheza vizuri sana, licha ya kwamba walifungwa na Cameroon, wataendelea kuwa watu wenye nafasi kubwa ya ubingwa. Pia wapo Ufaransa. Na Hispania, wanacheza vizuri sana. Wanapokuwa na mpira unakuwa kwenye umiliki wao kwa muda mrefu sana.”

Kuhusu Argentina, Messi alisema: “Argentina ina nguvu na siku zote ni miongoni mwa timu kubwa. Nafahamu kabla hatujaja kwenye fainali hizi tulikuwa moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa na hilo linatupasa tulithibitishe. Na bahati nzuri tunaenda taratibu.”

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUTINGA FAINAL CAF ....SARPONG ATAMANAI KURUDI KUKIPIGA TENA ...