Home Habari za michezo WAKATI BALEKE AKIANZA MBIO MAPEMA…KIPA MPYA SIMBA APEWA ONYO…

WAKATI BALEKE AKIANZA MBIO MAPEMA…KIPA MPYA SIMBA APEWA ONYO…

Habari za Simba

Ligi Kuu ya NBC imekamilisha mzungungo wa tatu na mpaka sasa tayari rekodi zimeanza kuwekwa kwa timu na wachezaji.

Hii ndio orodha ya waweka nyavu mpaka sasa ambapo Jean Baleke wa Simba ndiye kinara:

1. Jean Baleke (Simba) – 5

2. Feisal Salum (Azam) – 3

3. Aziz Ki (Yanga) – 2

4. Mudathir Yahya (Yanga) – 2

5. Max Nzengeli (Yanga) – 2

6. Prince Dube (Azam) – 2

7. Adam Adam (Mashujaa) – 2

8. Matheo Anthony (Mtibwa) – 2

9. Idd Nado ( Azam) – 2

MASHABIKI WAMKATAA AYOUB..

Shabiki wa Klabu ya Simba, Nabii Meja anasema kuwa siku akiwa nadaka golini kipa mpya wa Simba SC, Ayoub Lakred yeye huwa anaangalia mpira huku akiwa ana Panadol pembeni ili kupoza maumivu.

Meja amesema hayo akidai kuwa Lakred ambaye ni raia wa Morocco hana ubora wa kudakia Simba lakini anashangaa amesajiliwaje kwenye kikosi hicho na kupangwa kucheza.

“Nafasi ambazo wanampa huyu kipa wa sasa wa Simba, Ayoub huwa ninaangalia huku nikiwa na Panadol. Yani ninaumia, inawezekana vipi benchi zima la ufundi, timu nzima ya Simba Sc wanashinda kuona kwamba huyu kipa ana mapungufu kuliko mapungufu yenyewe?

“Ile mipira hata mtoto wangu anadaka. Tuwe serious, yule kipa ana uwezo mdogo sana, hata mashabiki wachukie, viongozi wa Simba wachukie lakini ukweli ni kwamba Ayoub ana uwezo mdogo sana wa kudaka, yani kudaka kuzuia ana uwezo mdogo.

“Jana yalipigwa mashuti machache na Coastal Union kwa sababu tu walikuwa hawawezi kuingia sana kwenye boksi la Simba. Walipiga mashuti mawili matatu lakini hakuweza kuyatendea haki, hata namna anavyo-punch mpira unaona kabisa kwamba hana uwezo,” amesema Nabii Meja.

SOMA NA HII  PENATI YA KAGERE NA UTAMU WA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA....UKWELI UKO HAPA

2 COMMENTS