Home Habari za michezo MCHAMBUZI:- KIPA MWARABU SIMBA BADO SANA…ANAKOSA BAADHI YA VITU…

MCHAMBUZI:- KIPA MWARABU SIMBA BADO SANA…ANAKOSA BAADHI YA VITU…

Habari za Simba SC

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia East Africa Radio, Abissay Stephen amesema kuwa kipa mpya wa Simba SC, Ayoub Lakred bado hajawa na fitness ya kutosha kuweza kutumikia majukumu yake kwenye timu yake hiyo mpya.

Abissay amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC na Coastal Union ya Tanga jana pale Uhuru Stadium na Msimbazi kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0.

Ayoub alionekana bado anafanya makosa ambayo hata hivyo Coastal hawakunufaika nayo, jambo ambalo limekuwa likiibua maswali miongoni mwa mashabiki wa Simba wakihoji uwezo wa kipa huyo aliyesajiliwa kutokea Morocco.

Mabao yote ya Simba yalifungwa na mchambuliaji wao, Jean Baleke raia wa Congo DR dakika ya 6, dakika ya 12 na dakika ta 40 kwa mkwaju wa penati.

“Mimi nikimwona Ayoub namuona kwamba ni kipa ambaye fitness yake bado haijawa tayari kwa mtazamo wangu mimi, anavyo catch unaona bado akili yake anavyofikiria na mwili havijaunganika kuwa kwenye ile fitness ya kusema kwamba “huyu ashindane.

“Kinachoendelea ni kwamba… okay wewe ni kipa ambaye umetoka ligi kubwa kuna vitu unavyo hebu ngoja tuone utaonesha kitu gani.

“Kwa hiyo hata ile mistake aliyofanya kule Ndola Zambia inaakisi kwamba kipa mentality yake haikuwa tayari sana, body language yakee, ila tu naona ili kumtafutia fitness kwenye mechi ndio maana wanampa nafasi anacheza,” amesema Abissay Stephen.

SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI KUHUSU DILI LA KINZUBI KUTUA YANGA...GSM AACHA BALAA KWA KATUMBI..