Home news SAKATA LA MKATABA WA GSM NA LIGI KUU..KARIA AIBUKA NA KUTOA KAULI...

SAKATA LA MKATABA WA GSM NA LIGI KUU..KARIA AIBUKA NA KUTOA KAULI HIII….AKANA KUHUSIKA…

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amekiri shirikisho hilo lipo kwenye mazungumzo na Kampuni ya GSM iliyotangaza kujitoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara kwa lengo la kumbakisha mdhamini huyo.


GSM ilitangaza kujitoa kupitia kwa Ofisa Biashara wake, Allan Chonjo aliyethibitisha wamejiondoa kwenye udhamini mwenza baada ya TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kusimamia matakwa yaliyopo kwenye mkataba walioingia na wiki iliyopita tuliripoti kuwepo kwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili, huku baadhi ya vigogo wa shirikisho hilo wakificha, lakini jana Karia amekiri jambo hilo na linasimamiwa na kamati maalumu.

Karia aliliambia gazeti la Mwanaspoti, mazungumzo yanaendelea, japo yeye hahusiki moja kwa moja na kwamba anasubiria yakamilike kabla ya kupewa taarifa.
SOMA NA HII  WIKIENDI YA KIBABE HII HAPA....ODDS ZA KUSHIBA ZA MERIDIANBET ZINAKUPA UHAKIKA WA MAMILIONI...